Upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo unamtuhumu rais wa nchi hiyo Felix Tshikedi kuanza kufanya kampeni za mapema kuelekea uchaguzi wa mwaka unaokuja kinyume na sheria. Kwenye Kinagaubaga ,Rashid Chilumba amemkaribisha Patrick Mundeke, mmoja ya washauri wa mwanasiasa wa upinzani Moise Katumbi.