Viongozi kadhaa wa kiafrika walihuzuria wiki iliopita (27.08.2021) mkutano wa kilele wa marais na viongozi wa serikali za nchi za Afrika na Ujerumani. Kipi Afrika mashariki itegemee baada ya mkutano huo, na je, wawekezaji wa Kijerumani wamevutiwa na bara hilo?
Katika makala hii ya Kinagaubaga, Saleh Mwanamilongo amezungumza na Dokta Abdallah Saleh Possi, balozi wa Tanzania nchini Ujerumani.