Kimbunga Man-yi chaipiga Ufilipino
17 Novemba 2024Idara ya huduma ya hali ya hewa imetahadharisha kuhusu hatari ya kutokea mafuriko, maporomoko ya ardhi na mawimbi makubwa wakati taifa hilo linapoendelea kukumbwa na dhoruba hiyo kali.
Zaidi ya watu milioni 1.2 walilazimika kuyakimbia maakazi yao mapema huku tahadhari kubwa ikitolewa na watabiri wa hali ya hewa juu ya athari za kutishia maisha ya watu kutokana na dhoruba hiyo yenye nguvu, ambayo inafuatia mkondo usio wa kawaida kwa sababu ya hali mbaya ya hewa.
Soma zaidi: Kimbunga Man-yi chapiga vikali nchini Ufilipino
Kwa mujibu wa mtabiri wa hali ya hewa Junie Ruiz, alipozungumza na shirika la habari la AFP alisema kimbunga Man-yi kilivuma kwa upepo wa kasi ya kilomita 185 kwa saa wakati kilipotua kwa mara ya pili kwenye mji wa Dipaculao ulio katika jimbo la Aurora kwenye kisiwa cha Luzon nchini Ufilipino.