Kimbunga chauwa zaidi ya watu 150 Ufilipino
22 Juni 2008Matangazo
Kimbunga hicho pia kimewapotezea makaazi wengine maelfu kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi.
Watu 59 wameuwawa katika jimbo la kati la Iloilo lilioko kilomita 560 kusini mwa mji mkuu wa Manila ambapo miji kadhaa imefurikwa na maji wakati kimbunga hicho Fengshen kilipopiga kwanza eneo hilo hapo jana.
Gavana wa Iloilo Neil Tupas ametangaza jimbo hilo kuwa katika hali ya maafa wakati akielezea hofu yake kwamba idadi ya vifo inaweza kupindukia watu 100 kutokana na maeneo mengi kuwa hayawezi kufikiwa.
Kimbunga hicho kimesababisha mvua mkubwa na upepo mkali unaosafiri kilomita 120 kwa saa ambao pia umekata nguvu za umeme na kusababisha uharibifu mkubwa sana kwa majengo.