1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kim Jung Ill achaguliwa tena kuiongoza Korea Kaskazini

Aboubakary Jumaa Liongo9 Aprili 2009

Bunge la Korea kaskazini limemchagua tena Kim Jon-il kuwa Mkuu wa Jeshi, nakuonekana kwake kumekuja wakati nchi hiyo ikisherehekea kile ilichokiita ushindi baada ya kurusha Satelite yake katika anga za juu hivi karibuni

https://p.dw.com/p/HTWq
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jung llPicha: AP


Shirika la Habari la Korea Kaskazini -KCNA- limeripoti kuwa kikao cha kwanza cha bunge la 12 la Jamhuri ya Watu wa Korea, kilichofanyika leo kimemchagua Kim Jong il, Mwenyekiti wa Tume ya Ulinzi, chombo ambacho kinanguvu kubwa katika serikali ya nchi hiyo.


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Ulinzi ndipo hatamu za uongozi wa Korea kaskazini zilipo, tume hiyo ndiyo iliyomteua mwasisi wa taifa hilo Kim Il Sung ambaye ndio baba wa kiongozi huyo wa sasa wa Korea Kaskazini.


Bado haijafahamika wazi, kama kiongozi huyo wa Korea kaskazini, ambaye ameongoza nchi hiyo tangu mwezi Julai mwaka 1994, baada ya kifo cha baba yake, Kim II Sung, alikuwepo katika kikao hicho, ambapo ni kawaida kuhudhuria kwake wakati wa ufunguzi wa kikao cha bunge.

Kim Jong Il Machthaber Nord Korea
Kim Jung llPicha: AP

Korea kaskazini imeweza kumuibua tena kiongozi wake huyo kutoka katika ugonjwa kupitia ripoti walizokuwa wakizionesha, akifanya ziara katika viwanda na vituo vya kijeshi.


Kim mwenye miaka 67, ameonekana kutoonekana hadharani katika matukio makubwa baada ya kuhisiwa kupatwa na ugonjwa wa kiharusi mwezi Oktoba mwaka jana, hali ambayo ilizua maswali juu ya nguvu za madaraka yake katika utawala wa kikomunisti ulioandamwa na ushawishi wa familia yake.

Kuchaguliwa huko kwa mara ya tatu kwa kiongozi huyo wa Korea kaskazini ni kawaida, katika nchi ya chama kimoja, lakini wachambuzi wa mambo wanasema ni kushikiza nafasi na madaraka katika mfumo wa utawala, baada ya miaka 67, ambapo kwa mujibu wa Maafisa usalama wa Korea kusini alikuwa akiumwa ugonjwa wa kiharusi mwaka uliopita.

Katika Kikao cha kwanza cha Bunge jipya la Korea kaskazini, ambalo huchaguliwa kila baada ya miaka mitano, kunatarajiwa pia kuwepo mabadiliko ndani ya tume hiyo ya taifa ya ulinzi kama vile kupanuliwa kwa njia ya kuongeza nguvu zaidi za kiongozi huyo.


Watafiti wanasema mabadiliko hayo na uteuzi utakaofanywa yanaweza kutengeneza njia kwa mmoja wa watoto watatu wa kiongozi huyo na kuweza kurithi nafasi hiyo.


Nordkorea und Japan land-to-air missiles
Picha: AP

Hatua ya Korea kaskazini kumchagua tena Kim Jong il kuongoza nchi hiyo, inakuja wakati ambao Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa kukubaliana juu ya hatua ya kuichukulia nchi hiyo kutokana na hatua yake ya kupeleka Satelite anga za juu, hatua ambayo inaonekana kama ni kuficha jaribio lake la kombora, jambo ambalo limesababisha Seneta John McCain wa Marekani kuishinikiza China, mshirika mkubwa wa Korea kaskazini kuchukua hatua zaidi kudhibiti nchi hiyo.


Seneta McCain ameyasema hayo baada ya kukutana na Waziri wa Ulinzi wa China, mjini Beijing.


Mwandishi: Halima Nyanza

Mhariri: Mohammed Abdulrahman