SiasaKorea Kaskazini
Kim Jong Un akutana na Waziri wa maliasili wa Urusi
19 Novemba 2024Matangazo
Hii inachukuliwa kama ishara ya hivi punde ya kuimarika kwa mahusiano kati ya Pyongyang na Moscow. Wakati wa mkutano huo, Kim amesema kuna ulazima wa kutanua ushirikiano katika sekta ya biashara, sayansi na teknolojia, kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa nchi hizo mbili.
Soma pia: Korea Kaskazini yaidhinisha mkataba wa kihistoria wa ulinzi na Urusi
Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol, amezitaka Urusi na Korea Kaskazini kukomesha ushirikiano wao wa kijeshi ambao ameutaja kuwa haramu. Kwa upande wake Pyongyang imekosoa ushirikiano wa pande tatu kati ya Korea Kusini, Marekani na Japan na kusema unasababisha hali ya mifarakano na makabiliano.