Kilele cha miaka 50 ya DW
22 Februari 2013Mkuu wa idhaa hii, Andrea Schmidt akiwa na baadhi ya wafanyakazi, alikuwa na mkutano na waandishi wa habari, mkutano ambao umehudhuriwa na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Klaus-Peter Brandes, ambao wote kwa pamoja wamejadili nafasi ya vyombo vya habari kwenye ujenzi wa jamii imara.
Maadhimisho hayo yanafanyika sambamba na mdahalo maalumu ulipangwa kufanyika siku ya ijumaa ukuwaleta pamoja magwiji wa uandishi wa habari pamoja na wanaharakati wa maendeleo.
Mada mbalimbali kuwasilishwa
Chini ya maudhui isemayo "Maarifa na Mwamko" watoa mada kwenye mjadala huo wanatazamia kujadilia kwa kina nafasi ya vyombo vya habari katika ujenzi wa jamii bora na ukuzaji wa masuala ya haki za binadamu na demokrasia. Hatua ambayo itatanguliwa na hotuba maalum kutoka kwa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Klaus-Peter Brandes na Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili DW, Andrea Schmidt.
DW ambayo ilianza kupeperusha matangazao yake miaka 50 iliyopita wakati wa vugu vugu la vita baridi, inajivunia mafanikio iliyoyopata katika eneo la afrika mashairiki na kati na hata maeneo mengine duniani yanayozungumza lugha ya Kiswahili.
Kiswahili kimekuwa duniani
Akizungumzia hatua ya DW kuadhimisha sherehe hizi nchini Tanzania, Naibu Mkuu wa idhaa ya Kiswahili Mohamed Abdulrahman alielezea sababu za maadhimisho hayo kufanyika Dar es Salaam. "Kwanza tunawasikilizaji wengi Tanzania. Tanzania tunaweza kusema ni chimbuko la lugha ya Kiswahili, nia vilevile imefanya mengi katika kukiendeleza Kiswahili na kufikia hatua ambayo hii leo lugha hiyo sio tu kwamba inazunguzwa katika nchi ambazo zinazungumza katika eneo hilo la Afrika maashariki na Kati, kinazungumzwa hata katia nchi za Ulaya kwa maana ya kwamba vyuo vikuu takriabani vyote barani Ulaya na Marekani kwa sehemu fulani vina idara mbalimbali za lugha na miongoni mwa lugha hizo ni Kiswahili". Alisema mtangazaji huyo mkongwe.
DW ambayo huendeshwa kwa bajeti ya serikali ya Ujerumani inakusanya jumla ya wafanyakazi 1,500 waliogawika katika vitengo mbalimbali na katima msimu wa mwaka ulipita alipata kiasi cha euro milioni 270 kwa ajili ya kuendesha shughuli zake za utangazaji duniani kote.
Balozi asisitiza uhuru wa habari
Akizungumzia kuhusu uhuru wa vyombo vya habari kwa nchi za Afrika, Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Klaus Peter Brandes alisema kuwa nchi za Umoja wa Ulaya zinapendelea kuona uhuru huo unaheshimika.
Alisema kuwa Umoja wa Ulaya ambayo moja ya nguzu yake muhimu na kusimamia haki za binadamu na uhuru wa Maoni, hivyo Ujerumani ikiwe sehemu ya Umoja huo itaendelea kutilia mkazo umuhumu wa kuheshimiwa uhuru huo wa maoni.
Uhuru wa vyombo vya habari ni moja ya nguzo muhimu kunapotajwa dhana ya maendeleo na ukuaji wa demokrasia
Mwishoni mwa mdahalo huo washiriki watapa fursa ya kujadiliana haya na yale kuhusiana na utendaji wa vyombo vya habari. Sikiliza taarifa ya George Njogopa kutoka Dar es Salalaam. Sikiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya kusikiliza masikioni hapo chini.
Mwandishi:George Njogopa
Mhariri: Yusuf Saumu