Wakati maandamano yanaendelea kwa ajili ya kuushinikiza ujumbe wa Umoja wa Mataifa MONUSCO uondoke DRC, jana Jumapili kulitokea sintofahamu kwenye mpaka kati ya Kongo na Uganda. Askari wa Umoja wa mataifa walibomoa kizuizi cha serikali kwa risasi na kuingia nchini Kongo. Katika purukushani hizo watu 8 waliuawa na wengine 14 walijeruhiwa vibaya. Sikiliza ripoti ya John Kanyunyu kutoka Beni.