1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kikosi cha Umoja wa Mataifa chaanza kazi Darfur

31 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CiWd

Umoja wa Afrika umekabidhi madaraka kwa kikosi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan.

Jumuiya ya kimataifa ina matumaini kwamba kikosi hicho kitasaidia kumaliza machafuko katika eneo la Darfur.

Sherehe ya kukabidhi madaraka imefanyika katika makao makuu mapya ya tume hiyo nje ya mji mkuu wa Darfur Kaskazini wa El Fasher na kumaliza shinikizo la kimataifa dhidi ya rais wa Sudan, Omar el Bashir.

Lakini kikosi hicho kipya kina idadi ya wanajeshi 9,000 badala ya idadi ya wanajeshi 26,000.

Rais wa Sudan amekuwa akitatiza juhudi za kukipeleka kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa katika eneo la Darfur na nchi za magharibi hazijakuwa zikipeleka helikopta kwa kasi inayotakikana ili kufanikisha kazi ya kikosi hicho.

Wachambuzi ndani na nje ya Umoja wa Mataifa wanasema kikosi hicho hakitaweza kwa haraka kuboresha usalama katika eneo la Darfur.