SiasaChina
Bunge la China lafungua kikao chake cha kila mwaka
5 Machi 2024Matangazo
Kikao hicho kinachofanyika kwenye eneo linalofahamika kama "Ukumbi wa Umma wa China" katikati mwa mji mkuu Beijing, kikihudhuriwa na maelfu ya wawakilishi wa kuchaguliwa kutoka kila pembe ya taifa hilo.
Kwenye hotuba yake Waziri Mkuu Qiang amesema China inalenga kufikia ukuaji uchumi wa asilimia 5 mwaka huu kupitia mpango wa mageuzi kwenye sekta za maendeleo pamoja na kupunguza matumizi holela ya serikali za mitaa.
Ama kuhusu suala la Taiwan, Qiang, amesema Beijing itakuwa imara kuelekea kutimiza dhamira ya kuuungana tena na kisiwa hicho chenye utawala wake wa ndani, ambacho kimekuwa kitovu cha mvutano kati ya China na hasimu wake Marekani.