1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kifo cha McCain na ziara ya Papa Francis Magazetini

Oumilkheir Hamidou
27 Agosti 2018

Kifo cha mwanasiasa, shujaa wa vita vya Vietnam, John McCain, ziara ya kiongozi wa kanisa katoliki Ireland na mvutano kati ya waziri wa mambo ya ndani wa Italia Salvini na Umoja wa ulaya kuhusu wakimbizi magazetini

https://p.dw.com/p/33pTF
USA TV-Duell zwischen Obama und McCain 2008
Picha: picture-alliance/ dpa/C. Berkey

Tunaanzia Marekani ambako risala za rambi rambi kutokana na kifo cha senetor wa muda mrefu wa jimbo la Arizona zinazidi kumiminika. Moyo wake wa kijasiri na maadili aliyokuwa akiyapigania ni miongoni mwa sifa zinazotajwa na viongozi sio tuu wa Marekani bali pia na kwengineko ulimwenguni. Vyombo vya habari pia vinamsifu, kama anavyoandika mhariri wa gazeti la "Rhein-Necker-Zeitung" la mjini Heidelberg: "Kwa kufafriki dunia John McCain, America imepotelewa na mwanasiasa muhimu kupita kiasi aliyekuwa na uwezo wa kujibisha ufidhuli wa Donald Trump. Kiongozi ambae baadhi ya wakati aliweza angalao kumpa uso mzandiki mwenye nguvu na mkubwa kupita wote ulimwenguni.

Ni kweli lakini kwamba alikuwa McCain aliyekifanya chama cha Republican cha Marekani kielemee zaidi  mrengo wa kulia. Aliridhia Sarah Palin wa chama cha Tea-Party awe makamo wake  katika kugombea kiti cha rais katika kampeni za uchaguzi dhidi ya Barack Obama. Kwasababu balaa lote hili limeanzia wakati ule, na kwa kuteuliwa bibi huyo. Bila ya Sarah Palin na chama cha Tea Party, maadili ya Republican yasingepungua kama hivi na kufika hadi ya kumfungulia njia Donald Trump ya kuingia ikulu ya White House."

Papa Francis aomba radhi kwa maovu yaliyofanyika

Kongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni Papa Francis amemaliza ziara yake katika jamhuri ya Ireland-ziara iliyogubikwa na kashfa za kudhalilishwa kingono watoto na baadhi ya mapadri nchini humo. Gazeti la  Reutlinger General-Anzeiger linaandika: "Kanisa linabidi lichunguze visa hivyo vya uhalifu na kuhakikisha wahalifu wanapata adhabu inayowastahiki. Makardinal na maaskofu waliosaidia kuficha yaliyotokea nao pia wafikishwe mahakamani. Kupokonywa wadhifa wao  kwa aibu viongozi hao wa kanisa itakuwa hatua mojawapo japo ndogo anayoweza kufanya Papa Francis.

 Kwa wakati wote ambao Papa Francis atashindwa kuleta hali ya uwazi katika kadhia hiyo inayosababisha machungu ndipo nao ukuta wa taasisi huyo utakapozidi kulega lega. Na bila ya mageuzi bayana, asitegemee Papa Francis kwamba radhi aliyoiomba kwa niaba ya kanisa itasaidia kitu."

Waziri wa mambo ya ndanai wa Italia atunisha misuli

Mada yetu ya mwisho magazetini inatukisha Italia kumulika mvutano kati ya nchi hiyo na Umoja wa Ulaya kuhusu wahamiaji. Gazeti la Südwest-Presse" linaandika: "Hii haijawahi kushuhudiwa kwamba  nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya inajaribu kutumia vitisho ili kulifikia lengo lake ndani ya Umoja huo. Hata hivyo kwa kutumia mbinu hizo  Italia imeweza kufanikiwa-mamia kadhaa ya wakimbizi wamehamishiwa katika nchi nyengine za Umoja wa ulaya-mfano wa kile kisa cha Diciotti. Waziri wa mambo ya ndani Salvini aliwakatalia ruhusa ya kuingia nchini humo, uamuzi uliopelekea mwendesha mashitaka kuchunguza uwezekano wa kumfikisha mahakamani Ukosefu wa utaratibu wa pamoja wa kugawana wakimbizi miongoni mwa nchi za umoja wa ulaya ndio chanmzo cha ufanisi huo.

 

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri