1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Kiev yahamisha wagonjwa ikihofia mashambulizi ya Urusi

27 Aprili 2024

Mamlaka ya jiji la Kiev jana Ijumaa iliamuru kuondolewa mara moja wagonjwa katika zake hospitali mbili, kutokana na hofu ya uwezekano wa shambulizi la kombora la Urusi.

https://p.dw.com/p/4fF9S
Rais Volodymyr Zelensky
Rais Volodymyr Zelensky amekuwa akihamasisha misaada zaidi ya kijeshi ili kumkabili adui yake UrusiPicha: Vladimir Shtanko/picture alliance /Anadolu

Mamlaka hizo za Ukraine zimesema hatua hiyo inafuatia video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, iliyoashiria shambulizi hilo la Urusi.

Wagonjwa hao wamehamishiwa kwenye hospitali nyingine na moja ya hospitali iliyoathiriwa ni ya watoto iliyopo Obolon, kaskazini mwa Kyiv.

Hata hivyo, mamlaka hizo zimesema kile kinachodaiwa kwenye video hiyo ya kwamba kuna wanajeshi kwenye hospitali ni uongo mtupu na uchokozi kwenye eneo la adui, huku ikiituhumu Urusi kueneza uwongo ili kuhalalisha mashambulizi inayoweza kuyafanya kwenye vituo vya afya.