Kiasi cha watu 30 wauwawa kwenye shambulio la bomu Algeria
9 Septemba 2007Matangazo
Takriban watu 30 wameuwawa na wengine wengi wamejeruhiwa baada ya bomu lililotegwa ndani ya gari kulipuka katika kambi ya jeshi inayoishi maafisa wa ulinzi wa eneo la pwani nchini Algeria.Mlipuko huo ulitokea katika mji wa Dellys kaskazini mwa pwani kilomita 50 kutoka mjini Algiers.
Shambulio hilo la bomu lililodaiwa kufanywa na kundi la kigaidi la Alqaeda nchini humo lilitokea siku mbili baada ya shambulio jingine kutokea lililowauwa kiasi cha watu 20.Shambulio hilo lilifanywa dhidi ya umati wa watu waliokuwa wamesisimama wakisubiri kumlaki rais Abdelaziz Bouteflika aliyekuwa akitembelea mashariki mwa nchi hiyo.