1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Khedira kuihama Real Madrid

27 Machi 2015

Kiungo wa Ujerumani Sami Khedira amesema ataondoka klabu ya Uhispania Real Madrid wakati mkataba wake utakapokamilika mwishoni mwa msimu huu.

https://p.dw.com/p/1Eya3
Real Madrid Sami Khedira
Picha: Jose Jordan/AFP/Getty Images

Khedira mwenye umri wa miaka 27 alijiunga na Real mwaka wa 2010 kutoka klabu ya Stuttgart, ambapo ameisaidia klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Ulaya. Kwa sasa kuna ripoti kuwa anapanga kujiunga na klabu ya Bundesliga, Schalke 04.

Amesema uamuzi wake unatokana na dhamira ya kutaka kujiimarisha kama mchezaji na siyo kwa sababu haipendi Real Madrid. Ameongeza kuwa kwa sasa hajafanya mazungumzo na klabu yoyote. Timu za ligi ya Premier Chelsea na Arsenal pia zimehusishwa na nyota huyo wa Real.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu