KHARTOUM.Maandamano kupinga ziara ya naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani
28 Agosti 2006Matangazo
Ziara ya naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani nchini Sudan imekumbwa na maandamano ya watu wanao pinga ziara hiyo.
Sudan bado inapinga pendekezo la kuwapeleka wanajeshi wa kimataifa wa kulinda amani katika jimbo la Darfur.
Takriban wanafunzi 100 wameandamana katika ubalozi wa Marekani mjini Khartoum kupinga ziara ya Bibi Jendayi Frazer naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani ambae pia anashughulikia maswala ya Afrika.
Naibu waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani anatarajiwa kukutana na wawakilishi wa baraza la usalama la umoja wa mataifa leo hii kujadili hali ya jimbo la Dafur nchini Sudan.
Juhudi za kutaka kuishwawishi Sudan ikubali pendekezo hilo zimekabiliwa na vikwazo.