KHARTOUM:Balozi wa Canada na Tume ya Umoja wa Ulaya wafurushwa
24 Agosti 2007Sudan imewafukuza balozi wa ngazi za juu wa Canada na mjumbe wa Tume ya Umoja wa Ulaya nchini mwake kwa walichokieleza kuwa wanaingilia masuala ya ndani.Wanadiplomasia hao wawili walitaarifiwa nyakati mbalimbali na kuwaeleza kuwa watu wasiotambulika nchini humo.Hayo ni kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Sudan Ali Al Sadeq.
Tume ya Umoja wa Ulaya kwa upande wake inathibitisha kuwa mwanadiplomasia huyo anayeongoza ujumbe wa tume hiyo Kent Degerfelt hakuwamo nchini Sudan wakati agizo hilo likitolewa.Bwana Kent Degerfelt alikuwa nab ado yuko likizo kwa wakati huu na amehudumu katika nafasi hiyo kwa muda mrefu. Bado haijulikani kwanini wanadiplomasia hao wawili waliagizwa kuondoka nchini Sudan ila mataifa mengi ya magharibi yamekuwa yakishtumu serikali ya Sudan hususan suala la eneo la Darfur linalozongwa na ghasia.