1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM: Usalama na misaada ya kiutu iimarishwe Sudan

29 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CF8t

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan amelitembelea eneo la kusini nchini Sudan.Lengo la ziara hiyo ni kuunga mkono makubaliano ya amani ya mwezi Januari.Makubaliano hayo kati ya serikali ya Khartoum na waasi kusini mwa nchi yamemaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miaka 21.Annan alipowasili eneo hilo la kusini,alikutana na umati wa watu waliokuwa wakimuomba msaada wa chakula.Lengo la ziara yake ya siku tatu nchini Sudan ni kuendeleza misaada ya kiutu na jitahada za usalama katika jimbo la magharibi la Darfur na vile vile kuimarisha makubaliano ya amani kati ya serikali na waasi kusini mwa nchi.Siku ya jumamosi,Annan alitembelea kambi kubwa kabisa ya wakimbizi huko Darfur.Amesema,Umoja wa Mataifa unapesa za kuweza kuchukua hatua katika jimbo la Darfur,lakini eneo la kusini lililoteketezwa kwa vita pia lisisahauliwe.