1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM: Ubakaji wa wanawake umezagaa Darfur

27 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CEzm

Wanawake wanaoishi katika kambi za wakimbizi katika jimbo la Darfur,nchini Sudan wangali wakikabiliwa na kitisho cha kubakwa.Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu usalama,iliyotolewa siku ya Jumamosi.Ripoti hiyo imesema,wafanyakazi wawili wa Kisudan wa shirika linalotoa misaada,walitekwa nyara na waasi. Ikaongezea kuwa siku ya jumanne,wanawake 5 kutoka kambi ya Kalma,nje ya mji mkuu wa jimbo la Darfur,Nyala walitekwa nyara na kubakwa walipokwenda kukusanya kuni.Makundi yanayotetea haki za binadamu yametuhumu kuwa mtindo wa kuwabaka wanawake umezagaa na hutumiwa makusudi kama silaha vitani.Kwa upande mwingine mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Sudan na waasi,yalikwama siku ya jumamosi baada ya kufunguliwa wiki mbili za nyuma nchini Nigeria.