1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Khalifa Haftar aapa kuendeleza mashambulizi kuelekea Tripoli

Daniel Gakuba
10 Januari 2020

Jenerali Khalifa Haftar na vikosi vyake waapa kuendeleza operesheni kuelekea Tripoli licha ya mwito wa Urusi na Uturuki kutaka mapigano yasitishwe ifikapo Januari 12.

https://p.dw.com/p/3VzD2
Libyen Khalifa Haftar
Picha: AFP/A. Doma

Vikosi vitiifu kwa jenerali Khalifa Haftar anayedhibiti eneo la mashariki mwa Libya, vimesema vitaendeleza operesheni kuelekea katika mji mkuu, Tripoli, licha ya mwito wa Urusi na Uturuki kutaka usitishwaji wa mapigani ifikapo Januari 12.

Vikosi hivyo vinavyojiita Jeshi la Taifa la Libya, LNA kwa kifupi, vimekaribisha juhudi za Urusi za kuleta amani na utengamano nchini Libya, lakini vimeapa kutoacha mashambulizi dhidi ya kile ilichokiita, ''kundi la kigaidi'' linaloungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Serikali ya mjini Tripoli inayoongozwa na waziri mkuu Fayez al-Serraj inatambuliwa na Umoja wa Mataifa kama serikali halali ya Libya, lakini haijawahi kuwa na ushawishi mkubwa nje ya mji mkuu huo.

Libya imekuwa katika hali ya vurugu, tangu kuangushwa kwa utawala wa kiongozi wake wa muda mrefu, Moamer Gaddafi mwaka 2011.