Kesi yaendelea dhidi ya waasi wa ADF
16 Februari 2017Matangazo
Kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya mahakama katika eneo hilo, Meya Bwanakawa Masumbuko Nyonyi alieko madarakani na ambae hajasimamishwa kazi atafikishwa kizimbani kutoa ushahidi baada ya kushukiwa kuwa ni mmoja wa viongozi wa kundi la kigaidi ADF. Kamanda wa ADF aliyemtaja Meya huyo kuwa ni mmoja wa viongozi wa ADF, alimtaja pia Jenerali Mundos, aliekuwa pia kamanda wa operesheni za kijeshi dhidi ya kundi hilo la ADF katika mji na wilaya ya Beni, pale yalipoanza mauwaji ya raia kwa kukatwa kwa mapanga. Raia zaidi ya elfu moja na mia tano wameuawa na wanamgambo wa kundi la ADF, kwa mjibu wa takwimu za mashirika ya kiraia.