Kesi ya mpiganaji wa jihadi kutoka Mali yasikilizwa ICC
14 Julai 2020Matangazo
Al-Hassan ag Abdoul Aziz Mohamed Ag Mahmoud, mwenye umri wa miaka 42, ameshitakiwa kwa uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu, ubakaji na utumwa wa kingono.
Mashitaka hayo yanaanzia wakati kundi la Waislamu wenye itikadi kali walipotumia mapambano ya kundi la kabila la Tuareg mwaka 2012 kuikamata miji iliyoko katika hali tete upange wa kaskazini nchini Mali.
Waendesha mashitaka katika mahakama mjini The Hague watatoa maelezo yao ya ufunguzi dhidi ya mtu waliyemwelezea katika kikao cha kabla kuwa aliwatesa sana wakaazi wa eneo hilo.