Kesi ya madhamana watatu wa chama tawala cha zamani nchini Rwanda iliyokua ianze jana mjini Arusha Tanzania imeakhirishwa
6 Septemba 2005Muendesha mashtaka wa mahakama ya kimataifa kuhusu Rwanda anapanga kuwahoji mashahidi 143 katika kesi dhidi ya viongozi watatu wa chama tawala cha zamani nchini Rwanda-Habari hizo zimetangazwa na shirika la habari Hirondelle.Kesi hiyo iliyokuaa ianze jana mjini Arusha Tanzania imeakhirishwa.Haijuliakni lini itasikilizwa.Kesi hiyo inawahusu viongozi watatu wa zamani wa chama cha MRND,mwenyekiti wa zamani Mathieu Ngirumpatse, makamo wake wa kwanza Edouard Karemera na katibu mkuu Joseph Nzirorera.Wote watatu ambao ni wa kutoka kabila la hutu wanakabiliwa na mashtaka ya kuhusika na mauwaji ya halaiki,uhalifu dhidi ya ubinaadam na uhalifu wa vita.Wanatuhumiwa kuwanajisi au kuamuru watu wanajisiwe wakati wa mauwaji ya halaiki kati ya april 6 na july 17 mwaka 1994.Wote watatu wanadai hawana hatia.