Sheria na HakiIsrael
Kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel yaanza leo The Hague
11 Januari 2024Matangazo
Kesi hiyo mbele ya mahakama ya haki ya Umoja wa Mataifa ICJ yenye makao yake makuu mjini The Hague, nchini Uholanzi imefunguliwa na Afrika Kusini, moja ya wakosoaji wakubwa wa operesheni ya kijeshi ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza.
Nchi hiyo inaitaka mahakama ya ICJ iyazingatie matendo ya Israel kwenye ardhi hiyo ya Wapalestina kuwa mauaji ya halaiki chini ya mkataba wa kimataifa wa kuzuia na kuadhibu makosa ya mauaji ya kimbari uliopitishwa mwaka 1948.
Mkataba huo unafafanua kwamba mauaji ya halaiki ni matendo yanayosababisha vifo vya watu wengi kwa lengo la kusambaratisha kwa sehemu au kwa jumla, taifa zima, kabila au jamiii ya watu wa rangi ama dini moja.