Kesi wanaoshukiwa kutaka kuipindua serikali Ujerumani yaanza
29 Aprili 2024Matangazo
Washukiwa wote kwenye kesi hiyo ni sehemu ya vuguvugu la siasa kali linajiita "Reichsbürger" wakidaiwa kupanga njama ya kupindua serikali ya Ujerumani.
Kundi hilo linaupinga mfumo wa serikali ya Ujerumani uliowekwa baada ya vita, likidai uliwekwa na kudhibitiwa na Madola washirika yenye nguvu yaliyoshinda Vita vya Pili vya Dunia.
Polisi walifichua njama hiyo katika msururu wa matukio ya msako uliofanywa nchi nzima mnamo Desemba 7, 2022. Takriban watu 25 walikamatwa na sasa wako kizuizini wakisubiri kesi zao. Zaidi ya bunduki 380 zilipatikana, pamoja na karibu silaha 150,000.
Washtakiwa hao tisa wanawakilishwa na mawakili 22, huku mashahidi zaidi ya 300 wakitajwa, wakiwemo askari polisi 270.