Shughuli ya kutoa chanjo ya COVID-19 imeanza rasmi nchini Kenya ambapo kundi la kwanza kuchanjwa ni wahudumu wa afya katika kaunti zote 47. Dozi millioni 1.02 za chanjo ya virusi vya corona ziliwasili siku ya Jumanne, na kuifanya Kenya kuwa moja ya mataifa ya mwanzo kupokea chanjo hiyo barani Afrika. Thelma Mwadzaya alihudhuria ufunguzi wa shughuli hiyo jijini Nairobi na kuandaa ripoti hii.