1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yawaombea wahanga wa shambulizi la Westgate

Admin.WagnerD1 Oktoba 2013

Ni siku 9 sasa tangu mkasa wa Shambulizi la magaidi kutokea katika Jumba la kibiashara la Westgate mjini Nairobi, Kenya. Serikali imeandaa maombi ya kitaifa yanayojumuisha dini zote kuombea usalama wa nchi

https://p.dw.com/p/19s7q
Picha: Reuters

Maombi hayo pia ni ya kuwafariji wale waliopoteza wapendwa wao kwenye shambulizi hilo la magaidi lililosababisha vifo vya watu 67 na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa.

Viongozi wa dini mbali mbali wamekusanyika katika uwanja wa jumba la KICC kwa maombi ya kitaifa kuombea nchi, manusura na jamaa za waliopoteza wapendwa wao kwenye shambulizi la magaidi Shambulizi hilo lililofanyika tarehe 22 mwezi huu. Maombi hayo yamehudhuriwa na wakuu wa serikali wakiongozwa na Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Rutto, mawaziri na wabunge.

Pia viongozi wa upinzani wa muungano wa CORD wakiongozwa na aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga akiandamana na viongozi wa vyama tanzu wa muungano huo, aliyekuwa makamu wa Rais Kalonzo Musyoka na wengineo walijumuika pamoja katika uwanja wa jumba la mikutano ya Kimataifa KICC.

Bado kuna maswali mengi yaanyostahili majibu kuhusu namna serikali ilivyolishughulikia shambulizi hilo
Bado kuna maswali mengi yaanyostahili majibu kuhusu namna serikali ilivyolishughulikia shambulizi hiloPicha: CARL DE SOUZA/AFP/Getty Images

Maombi hayo yanahudhuriwa na viongozi wa didi mbali mbali wakiwemo wakristo, Waislam, Wahindu na dindi nyinginezo. Viongozi wa dini ya kiislam wameendelea kukikashifu kitendo hicho cha magaidi na kusihi vyombo vya usalama kutohusisha ugaidi na Uislam.. Huku maombi hayo yakiendelea kundi la wataalam wa uchunguzi kutoka mataifa mbali mbali wanaendelea na uchunguzi wao katika jumba la Westgate Mall kutafuta ushahidi kuhusiana na shambulizi hilo.

Maafisa kutoka Uingereza, Ujerumani Marekani, Israel na Canada wakishirikiana na wenzao kutoka Kenya wanaendesha shughuli iliyoanza Jumatano iliyopita. Maswali mengi hadi sasa hayajapata majibu kuhusiana na shambulizi hilo lililodaiwa kuteklelezwa namagaidi wa kundi la Al-Shabaab walio na uhusiano na kundi la magaidi la Al-Qaeda. Washukiwa tisa bado wanahojiwa na polisi kuhusian na shambulizi hilo. Serikali imesema magaidi 5 waliuawa kwenye shambulizi hilo ingawaje hadi sasa hakuna hata maiti moja ya magaidi hao iliyotambuliwa.

Mwandishi: Alfred Kiti

Mhariri: Josephat Charo