Serikali ya Kenya imetuma ujumbe nchini Somalia kwa lengo la kutafuta suluhisho kwenye mpaka wa mataifa hayo. Hatua hiyo inajiri baada ya makabiliano kati ya jeshi la Somalia na wanajeshi wa jimbo la Juba kuvuka mipaka hadi nchini Kenya. Watu kadhaa walijeruhiwa kwenye makabiliano hayo katika jimbo la Mandera nchini Kenya huku mtu mmoja akiripotiwa kuuwawa.