1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yashambuliwa, 14 wajeruhiwa

Abdu Said Mtullya24 Oktoba 2011

Watu 14 wamejeruhiwa kutokana na mashambulizi yaliyofanywa kwenye klabu ya burudani jijini Nairobi usiku wa kuamkia leo huku kukiwa na taarifa za kuhusika kwa kundi la wanamgambo wa al-Shabaab katika mashambulizi hayo.

https://p.dw.com/p/12xUD
Wapiganaji wa Al-Shabaab.
Wapiganaji wa Al-Shabaab.Picha: AP

Mkuu wa Polisi ya mji huo, Eric Mugambi, amesema kuwa uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa guruneti lilirushwa ndani ya klabu hiyo. Shambulio hilo limetokea wiki moja baada ya majeshi ya Kenya kuvuka mpaka na kuingia Somalia ili kuanzisha mashambulio dhidi ya wapiganaji wenye itikadi kali ya Kiislamu wa Al- Shabaab. Wapiganaji hao walitishia kufanya mashambulio makubwa ya kulipiza kisasi dhidi ya Kenya ikiwa nchi hiyo haitayaondoa majeshi yake kutoka Somalia.