Serikali ya Kenya imeridhia kutekeleza amri ya mahakama ya Afrika iliyowaagiza kuirejeshea jamii asili ya Ogiek makao yao kwenye msitu wa Mau, hatua itakayohitimisha mizozo ya ardhi na maafa ya mara kwa mara. Serikali ilisema kwamba suluhu la kudumu litapatikana kwa kuzingatia haki za jamii zilizoko eneo hilo. Mwandishi wetu Wakio Mbogho kutoka Nakuru alituandalia taarifa hii.