1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yapiga marufuku makanisa yanayohusishwa na vifo

18 Agosti 2023

Mamlaka nchini Kenya zimepiga marufuku makanisa matano likiwemo kanisa la mshukiwa aliyewachochea zaidi ya waumini wake 400 kufunga hadi kufa.

https://p.dw.com/p/4VKih
Zaidi ya miili 400 imefukuliwa msituni Shakahola Pwani ya Kenya. Inadaiwa miili hiyo ni ya waumini waliopotoshwa kutokana na mafundisho potofu ya kanisa lenye utata kufunga hadi kufa.
Zaidi ya miili 400 imefukuliwa msituni Shakahola Pwani ya Kenya. Inadaiwa miili hiyo ni ya waumini waliopotoshwa kutokana na mafundisho potofu ya kanisa lenye utata kufunga hadi kufa.Picha: Stringer/REUTERS

Msajili wa mashirika nchini humo katika notisi iliyowekwa kwense gazeti la taifa amesema, leseni ya mhubiri Paul Nthenge Mackenzie wa kanisa la Good News International Ministries, ilifutiliwa mbali kuanzia Mei 19.

Huku kutokula kukionekana kuwa ndicho chanzo kikuu cha sehemu kubwa ya hao watu 400 waliofariki, ripoti za upasuaji zinaonyesha wengine wakiwemo watoto walinyongwa, kupigwa au kubanwa pumzi hadi kufa.

Mamlaka zimeyapiga marufuku makanisa mengine 4 pia likiwemo la New Life Prayer Centre and Church lake mhubiri Ezekiel Odero ambaye amehusishwa na Mackenzie.

Odero anachunguzwa kwa mashtaka kadhaa yakiwemo mauaji, itikadi kali na utakatishaji fedha.