Serikali ya Kenya imekariri msimamo wake wa kuzifunga kambi za wakimbizi kutokana na hofu ya usalama wa kitaifa. Katika kikao cha kukusanya maoni ya umma kinachoendeshwa na kamati ya Bunge, serikali imesema tayari wakimbizi laki tatu wamerejea makwao.