Kuna wasiwasi kuhusu iwapo mpango wa kuwapatanisha wakenya wa BBI utaifikia dhamira yake baada ya wakenya na viongozi kuonekana kugawanyika kuhusu ripoti ya mpango huo. Vijana ni kundi ambalo limelalamikia kutengwa kwa muda mrefu na ripoti ya BBI iliyosubiriwa kwa hamu na ghamu inakabidhiwa rais hii leo, wengi wao wanatumai itakuwa ya kuwafaa. Sikiliza ripoti ya Wakio Mbogho.