1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yajitayarisha kwa ripoti ya maridhiano ´BBI´

Admin.WagnerD26 Novemba 2019

Kuna wasiwasi kuhusu iwapo mpango wa kuwapatanisha wakenya wa BBI utaifikia dhamira yake baada ya wakenya na viongozi kuonekana kugawanyika kuhusu ripoti ya mpango huo.

https://p.dw.com/p/3Tk75
Kenia Präsident Uhuru Kenyatta und Oppositionsführer Raila Odinga in Nairobi
Picha: Reuters/T. Mukoya

Vijana ni kundi ambalo limelalamikia kutengwa kwa muda mrefu na ripoti ya BBI iliyosubiriwa kwa hamu na ghamu.

Ripoti hiyo inakabidhiwa kwa rais Uhuru Kenyatta hii leo Jumanne, huku vijana wengi wanatumai itakuwa ya kuwafaa.

Daniel Kimani mwenyekiti wa muungano wa vijana wanaofahamika kama ‘Nakuru Youths and Governance' uendeshaji wa serikali iliyopo umekuwa kero kwa vijana na hawana matumaini kama mpango huu utakuwa tofauti.

John Gachui kiongozi wa vijana kutoka eneo la Njoro amesema anataka ripoti ya BBI kuyaangazia maslahi ya vijana.

Mitandao ya kijamii yatumika 

Kenia Symbolbild Smartphones
Picha: Getty Images/AFP/Y. Chiba

Kupitia ‘Hashtags' za #BBIunitingKenyans na #RejectBBI Wakenya wameonyesha hisia mseto katika kuunga mkono na kupinga utekelezaji wa ripoti hiyo.

Baadhi wanasema inakikiuka misingi ya katiba, wengine wanadai inayumbisha mwelekeo wa serikali huku baadhi wakiiona kama njia ya kuimarisha maridhiano na uchumi wa taifa.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, mwanasiasa Kabando wa Kabando anaitaja ripoti ya BBI kama mwanzo mpya na mwanga wa matumaini kwa taifa la Kenya huku seneta Millicent Omanga akiwataka wakenya kuisubiri ripoti hiyo kwanza kabla ya kuanza kuzungumzia kuwapatanisha wakenya.

Kenia Nairobi Großdemonstration der Opposition
Picha: Reuters/B. Ratner

Mbunge wa Molo Kimani Kuria amesisitiza suala la kuwajumuisha vijana katika maswala ya uongozi kuangaziwa kwenye ripoti hiyo ni muhimu.

Kinara wa chama cha upinzani cha  ODM Raila Odinga atakuwepo kwenye hafla ya kuipokea ripoti ya BBI.

Jopokazi la BBI limeelezea kukusanya maoni katika kaunti zote 47 pamoja na maombi kutoka kwa mashirika ya umma.

Jopokazi hili iliundwa baada ya rais Kenyatta na Raila Odinga kuzika tofauti zao za kisiasa na kuamua kufanya kazi pamoja.