Kenya: Usalama ukoje kabla ya uchaguzi?
26 Julai 2017Zikiwa zimebakia siku 12 hadi siku ya uchaguzi mkuu nchini Kenya, Kaimu Waziri wa Usalama wa Ndani nchini humo, Fred Matiangi, amesema kila juhudi zimechukuliwa kuhakikisha kwamba taasisi za usalama nchini humo zitaweza kudhibiti hali ya utulivu katika maeneo yote ya nchi siku ya uchaguzi, tarehe 8 Agosti mwaka huu. Lakini katika baadhi ya maeneo, ikiwemo kaunti kadhaa za mikoa ya Pwani na Bonde la Ufa, wakazi wengi wameyahama makazi yao na vituo kadhaa vya kupigia kura haviwezi kufikiwa, kwa sababu za kiusalama-hayo yakiwa kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu, Human Rights Watch. DW imezungumza na mmoja wa maafisa wa shirika hilo, Audrey Wabwire, na kwanza anafafnua kwanini tathmini yao inatofautiana na hali inayoelezwa na waziri!