Kenya: Sharti wageni wathibitishe wamepata chanjo ya COVID
6 Desemba 2021Matangazo
Kulingana na waziri wa afya Mutahi Kagwe, raia wote wa kigeni watatakiwa kuthibitisha kuwa wamepokea chanjo dhidi ya ugonjwa wa Covid 19 kwanza ndipo waruhusiwe kuingia nchini katika hatua hii inayolenga anga za usafiri za kuingia nchini Kenya.
Waziri Kagwe amefafanua kuwa, hatua hii ni mojawapo ya mkakati wa serikali katika kudhibiti makali ya kirusi cha korona cha Omicron.
Itakumbukwa kuwa, serikali ya Kenya ilikuwa imeahidi, haitafunga mipaka yake licha ya kuibuka kwa kirusi cha Omicron.