Waziri wa usalama wa ndani wa Kenya ametoa msimamo mkali kuhusu mapambano na wahalifu wanaowaua watu wasiokuwa na hatia maeneo ya bonde la ufa, matukio ambayo yamechochewa na wizi wa mifugo unaohusishwa na uhaba wa viunga vya malisho. Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wameikosoa hatua hiyo wakihoji inatoa mwanya kwa ukiukaji wa haki za kibinadamu. Sikiliza ripoti ya Wakio Mbogho.