MigogoroKenya
Kenya na Uganda kusuluhisha mzozo wa Ethiopia na Somalia
30 Novemba 2024Matangazo
Ruto ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba hii ni kwa sababu usalama wa Somalia unachangia kwa kiasi kikubwa katika utulivu wa kikanda, na kuboresha mazingira ya uwekezaji na wafanyabiashara.
Uturuki imejaribu mara kadhaa kusuluhisha mzozo huo lakini haijafanikiwa.
Ethiopia yenye maelfu ya wanajeshi nchini Somalia wanaopambana na waasi wenye mafungamano na al-Qaeda imejikuta katika mzozo na serikali ya Mogadishu kufuatia mipango yake ya kujenga bandari katika jimbo lililojitenga la Somaliland, ili badala yake iweze kuisaidia kutambuliwa kimataifa.
Somalia inaipinga vikali hatua hiyo.