1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya na mzozo wa Somalia

23 Juni 2009

Rais wa Somalia, Sheikh Ahmed Shariff, alitangaza sheria ya hali ya hatari katika nchi yote ya Somalia, na akatoa mwito wa ujiingizaji wa nchi za nje katika nchi hiyo, zikiwemo nchi jirani.

https://p.dw.com/p/IXjR
Rais wa Somalia Sheikh Ahmed ShariffPicha: ap

Lakini madola ya nje yanasita sita zaidi ya kuliimarisha jeshi la kulinda amani la askari 4,300 wa kutoka nchi za Umoja wa Afrika, AU. Jeshi hilo la AU halijaweza hadi sasa kuzuia michafuko, na doria za jeshi hilo zimekuwa ni malengo ya wapiganaji wa Kiislamu na wanamgambo wa al-Shabab wanaodhibiti sehemu nyingi za Somalia.

Punde hivi Othman Miraji alizungumza na kamanda wa jeshi la AU katika Somalia, Meja-Jenerali Francis Okello, na alimuuliza jeshi lake liko katika hali gani hivi sasa huko Mogadishu:


Mahojiano: Othman Miraji/Meja-Jenerali Francis Okello

Mhariri: Mohamed Abdulrahman