1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya kuwasilisha ombi la pamoja la uwenyeji wa AFCON2027

15 Mei 2023

Kenya, Uganda na Tanzania zitawasilisha Jumatano wiki hii ombi la Pamoja la kuwa mwenyeji wa kuandaa kinyang'anyiro cha Kombe la Mataifa Afrika – AFCON 2027

https://p.dw.com/p/4RNN5
Fußball Africa Cup vor Finale | Senegal v Ägypten
Picha: MOHAMED ABD EL GHANY/REUTERS

Kenya, Uganda na Tanzania zitawasilisha Jumatano wiki hii ombi la Pamoja la kuwa mwenyeji wa kuandaa kinyang'anyiro cha Kombe la Mataifa Afrika – AFCON 2027. Hayo yamesemwa na Rais wa Kenya William Ruto ambaye amekutana leo na jopo linaloshughulikia ombi hilo likiongozwa na Waziri wa michezo Ababu Namwamba na Rais wa Shriikisho la kandanda Kenya – FKF Nick Mwendwa. Ombi hilo limepewa kichwa cha EAC Pamoja bid. "Tunatumai kuwa ombi letu la pamoja, litahamasisha sio tu nchi zetu zote kufuzu katika kinyang'anyiro cha 2027, bali pia kufanya vizuri Zaidi kupita mafanikio ya awali kutoka kwa mataifa binafsi. Pia tunanuia kuwasilisha ombi muhimu, ambalo litafaulu katika kutupa fursa ya kuifanya kenya, Uganda na Tanzania kuwa vitovu vya kuibuka tena kwa kandanda la kikanda, na barani Afrika."

Shirikisho la kandanda Afrika – CAF lilithibitisha kuwa limepokea tamko la nia ya nchi hizo tatu za Afrika Mashariki pamoja na maombi ya Algeria, Botswana na Misri.

Vyanzo