Bunge la Kenya limepitisha pendekezo la kuanzisha uchunguzi kuhusu shughuli za kikosi cha Jeshi la Uingereza nchini humo (Batuk) katika kaunti za Nanyuki na Laikipia. Uchunguzi huo utajikita kwenye mashitaka kuhusu shughuli za wanajeshi hao ikiwa ni pamoja na madai ya mauaji ya mwanamke wa eneo la Nanyuki mwaka 2012 na tukio la moto mkubwa katika mbuga ya Lolldaiga Hills mnamo mwaka 2021.