1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya imesaini mkataba wa dola bilioni 5 na China

20 Agosti 2013

Serikali ya Kenya, imesaini mkataba wa biashara na China jana (19.082013) wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa reli na mradi wa umeme.

https://p.dw.com/p/19SfF
Kenya's newly elected President Uhuru Kenyatta attends the Easter Mass at the Saint Austin's Catholic church in the capital Nairobi, March 31, 2013. Kenya's Supreme Court upheld Uhuru Kenyatta's presidential election victory on Saturday and his defeated rival accepted the ruling, helping douse tensions after tribal violence blighted the election five years ago. REUTERS/Thomas Mukoya (KENYA - Tags: POLITICS ELECTIONS)
Rais Uhuru KenyattaPicha: Reuters

Serikali ya Kenya, imesaini mkataba wa biashara na China jana (19.082013) wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa reli na mradi wa umeme. Hatua hiyo inaongeza wigo wa uhusiano na taifa hilo la taifa la bara la Asia lenye lengo la kupanua wigo wake wa uwekezaji barani Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika ofisi ya rais ya Kenya fedha hizo zitatumika katika mradi wa nishati, ujenzi wa kiwango bora cha reli itakayoiunganisha bandari ya Mombasa na mji wa mpakani wa taifa hilo, Malaba.

Aidha taarifa hiyo inaeleza kuwa kiwango kingine cha fedha kitatumika katika kustawisha hifadhi ya wanyamapori katika taifa hilo ambalo limegubikwa na vitendo vya ujangili, ambapo wahalifu wamekuwa wakiwauwa wanyama aina ya tembo na vifaru kwa ajili ya pembe zao. Bidhaa hizo soko lake kubwa lipo China ambapo zinatumika katika kutengenezea madawa na mapambo.

Maswali kuhusu fedha hizo

Hata hivyo haijawekwa wazi kama pesa hizi zitakuwa mkopo, msaada au kiasi kipya au sehemu ya makubaliano ya awali ambacho hakikutangazwa. Makubaliano hayo yamefikiwa mjini Beijing baada ya mazungumzo kati ya rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na rais wa China, Xi Jinping. Rais Kenyatta yupo katika ziara ya kikazi nchini China ambayo ilianza Jumapili iliyopita na itakayomaliza siku ya Ijumaa.

China's newly elected President and chairman of the Central Military Commission Xi Jinping (L) talks with China's Vice Premier Li Keqiang during the fourth plenary meeting of the first session of the 12th National People's Congress (NPC) in Beijing, March 14, 2013. REUTERS/China Daily (CHINA - Tags: POLITICS) CHINA OUT. NO COMMERCIAL OR EDITORIAL SALES IN CHINA
Rais wa China Xi JinpingPicha: Reuters

Wakati wa ziara yake barani Afrika mwezi Machi mwaka huu, rais Jinping aliahidi kuliendeleza bara la Afrika ikiwa majibu ya malengo ya taifa hilo kubwa kuendelea pia kujipatia malighafi. Mpaka sasa China ina nafasi kubwa katika miradi ya ujenzi ya miundombinu nchini Kenya na hasa katika miradi ya barabara.

Ziara hiyo ya Kenyatta ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake kwa raia wa Kenya katika kampeni zake za uchaguzi wa Machi 4 mwaka huu. Aliahidi kushirikiana na China kutokana na mataifa kama Marekani, Uingereza na baadhi katika bara la Ulaya kusema yatakuwa na mipaka katika ushirikiano wao na taifa lake kutokana na kiongozi huyo kukabiliwa na mashitaka katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, mjini The Hague, Uholanzi, kuhusu tuhuma za uhalifu dhidi ya ubinaadamu zilizotokea baada ya uchaguzi wa 2007. Hata hivyo Kenyatta na naibu wake William Ruto wamekana tuhuma hizo na wameahidi kusafisha majina yao mbele ya umma wa mataifa.

Kujua zaidi kuhusu taarifa hiyo bonyeza kitufe cha kusikilizia masikioni hapo chini ambapo Amina Abukar amezungumza na mchambuzi, Profesa Barrack Muluka

Mwandishi: Sudi Mnette/RTRE

Mhariri:Josephat Charo