Serikali nchini Kenya imetangaza kuwa mtu yeyote ambaye hatakuwa amepata chanjo ya kumkinga dhidi ya virusi vya Corona kuanzia tarehe 21 mwezi Disemba atakosa huduma muhimu za serikali. Akitangaza agizo hilo Waziri wa Afya nchini humo Mutahi Kagwe amesema kuwa kila Mkenya atahitajika kuonesha cheti cha chanjo kabla ya kupokea huduma yoyote ya serikali.