1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Kayishema akabiliwa na mashtaka 54 nchini Afrika ya Kusini

9 Juni 2023

Waendesha mashtaka wa Afrika Kusini wameongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya mashtaka dhidi ya afisa wa zamani wa polisi wa Rwanda Fulgence Kayishema.

https://p.dw.com/p/4SOVj
Fulgence Kayishema ambaye amekuwa akisakwa kwa zaidi ya miongo miwili alikamatwa nchini Afrika ya Kusini
Fulgence Kayishema ambaye amekuwa akisakwa kwa zaidi ya miongo miwili alikamatwa nchini Afrika ya KusiniPicha: Nic Bothma/REUTERS

Akiwa mafichoni kwa miongo miwili, Kayishema alikamatwa Mei 24 chini ya jina la uwongo kwenye shamba la zabibu huko Afrika Kusini ambapo, kulingana na mwendesha mashtaka, wakimbizi wanaofanya kazi huko walimtoa.

Sasa anakabiliwa na mashtaka 54 tofauti nchini Afrika Kusini yanayohusiana na makosa ya ulaghai na uhamiaji, kutoka matano ya awali, alisema msemaji wa waendesha mashtaka Eric Ntabazalila mjini Cape Town.

Vitambulisho vya uongo

Kayishema alikimbia sheria tangu 2001, wakati Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) ili mfungulia mashtaka kwa mauaji ya kimbari kwa madai ya kuamuru mauaji ya watu 2,000 waliojificha katika Kanisa Katoliki la Nyange.

Afisa huyo wa zamani wa polisi, alikanusha kuhusika kwa vyovyote wakati alipokuwa akizikiziza ufunguzi wa kesi yake mnamo Mei 26, ingawa alisema alisikitishwa na mauaji ya 1994. Mamlaka ya Kitaifa ya Mashtaka ya Afrika Kusini (NPA) imesema kwamba Kayishema alitumia utambulisho wa uongo kuomba hifadhi na hadhi ya ukimbizi nchini Afrika Kusini. Kayishema hajajibu mahakamani kwa mashtaka hayo ya Afrika Kusini.

Kifungo cha hadi miaka 15 jela 

Mahakama ya kimataifa kuhusu mauwaji ya kimbari Rwanda ayaendelea kuwasaka washukiwa wengine watatu
Mahakama ya kimataifa kuhusu mauwaji ya kimbari Rwanda ayaendelea kuwasaka washukiwa wengine watatuPicha: Ben Curtis/AP/picture alliance

Kesi hiyo ilisimamishwa hadi Juni 20 ili kuruhusu timu ya mawakili ya Kayishema kushauriana, ambapo anaweza kuomba kuachiliwa kwa dhamana.

Baadhi ya mashtaka ya hayo yanaweza kumfanya Kayishema kufungwa kwa hadi miaka 15, alisema Ntabazalila.

Kayishema pia anatarajiwa kurejeshwa Rwanda kuhukumiwa juu ya mashitaka ya mauaji ya kimbari ya ICTR, lakini hizo kesi bado hazijaanza, Ntabazalila alisema.

Takriban watu 800,000 wa kabila la Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliouawa wakati wa mauaji ya kimbari ya Rwanda, yaliyoratibiwa na watu wenye msimamo mkali chini ya utawala wa Wahutu. Kukamatwa kwa Fulgence Kayishema kumeacha watoro watatu pekee kufunguliwa mashtaka na mahakama ya kimataifa ambayo bado haijulikani walipo.

 

Reuters