1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kavanaugh na vijana wa CDU Magazetini

Oumilkheir Hamidou
8 Oktoba 2018

Kuapishwa mteule wa rais wa Marekani Brett Kavanaugh kuwa jaji wa mahakama kuu na siku ya vijana wa CDU ni miongoni mwa mada magazetini.

https://p.dw.com/p/369m3
USA Senat bestätigt umstrittenen Richterkandidaten Kavanaugh | Innenraum mit Abstimmungsergebnis
Picha: Reuters/Senate TV

Tunaanzia Marekani ambako licha ya madai ya ubakaji, baraza la Seneti la Marekani limemchagua kwa sauti 50 dhidi ya 48 jaji Brett Kavanaugh awe mwanachama wa korti kuu nchini humo. Kura ya Kavanaugh imeichafulia hadhi yake taasisi hiyo muhimu ya Marekani linaandika gazeti la mjini Dresden-"Sächsische Zeitung."Kuteuliwa Kavanaugh halikuwa suala la kumtafuta mwenye ujuzi au la maadili, lilikuwa suala la kuoneshana  nani ana nguvu. Republican walitaka kujionyesha wana msimamo mmoja kuelekea uchaguzi wa mwezi unaokuja wa November. Na muhimu zaidi, uamuzi wa baraza la Seneti utaselelea hata baada ya mhula wa Trump kumalizika."

Majuba meusi yameingia dowa

Gazeti la "Badische Neueste Nachrichrichten" linakwenda mbali zaidi na kuandika: "Kwa kuchaguliwa Kavanaugh, imetoweka pia ile ndoto, jopo hilo muhimu la wanasheria tisa wake kwa waume na majuba yao meusi , wangeweza kujiepusha na malumbano ya kisiasa. Kwa kujiunga mtu kama huyo, korti kuu hiyo imepoteza nembo yake inayoilingasnisha na baraza la wenye busara, baraza lisiloelemea upande wowote, na huru."

Vijana wa CDU wadai mageuzi

Katika mkutano wa tawi la vijana wa chama cha Christian Democratic Union-CDU- uliofanyika mwishoni mwa wiki katika mji wa kaskazini wa Kiel, kero za vijana hazijakosekana. Sauti zilihanikiza pia kudai mhula wa kansela uwe na kikomo. Gazeti la "MItteldeutsche Zeiting" linaandika: "Ni kiroja kikubwa hiki kwamba chama kilichooongozwa na Konrad Adenauer, Helmut Kohl na sasa Angela Merkel kinakabiliwa na shinikizo kama hilo. Hali hiyo inabainisha jinsi nguvu  zilivyowaishia. Hawawezi kufanya lolote dhidi ya viongozi wao, labda mapinduzi  na hayo hayana mwisho mwema. Miito ya kuwekea kikomo mhula wa kansela unamaanisha kinyang'anyiro cha kuwania madaraka kinatangulizwa mbele badala ya majukumu makubwa yaliyoko."

Hakuna wa kushindana na Angela Merkel

Gazeti la "Ludwigsburger Kreiszeitung" linahisi vishindo vya Kiel havikumtikisa kansela Angela Merkel.Ggazeti linaendelea kuandika: "Kansela amepasi mitihani yote ya Kiel. Hakutikisika. Amewashinda kutokana na miito  yake kudai idadi ya wanawake izidishwe katika uongozi wa tawi la vijana na wito wake wa kutangulizwa mbele majukumu muhimu ya siku za mbele. Amepasi pia kwasababu kwasasa hakuna yeyote anaeweza kushindana nae katika kuania uongozi wa CDU. Na mjini Kiel pia hakuchomoza hata kama makofi aliyopigiwa mwenyekiti mpya wa kundi la wabunge wa CDU/CSU Ralph Brinkhaus yamedhihirisha wana kiu cha mageuzi."

.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri: Iddi Ssessanga