Katuni za Umoja wa Afrika
Kila mwaka "Third World Journalist Net" wanaandaa mashindano ya kimataifa ya uchoraji kantuni. Shindano la mwaka huu limehusisha mada kuhusu " Miaka 50 ya umoja wa Afrika"
Tuzo ya kwanza ya AU bila ya magurudumu
Katuni iliyopewa jina " Je tumeshafika?" imechorwa na mchoraji wa Afrika Kusini John Swanepoel na Jonh Curtis. Katika nchi yao wanajulikana kama "Dr. Jack & Curtis." Wachoraji hao wameshika nafasi ya kwanza katika shindano la tatu kwa mwaka huu la uchoraji katuni la Ujerumani " Third World Journalist Net" Kwa mwaka huu, mada kuu ya shindano hilo la kimataifa ilikuwa "Miaka 50 ya umoja wa Afrika"
Tundu katika sehemu ya pili
"Umoja ni muhimu kwa kudumisha Afrika." Hivyo ndivyo ambavyo Victor Ndula kutoka Kenya alivyoupa mchoro wake jina. Alipata nafasi ya katika shindano la kuchora katuni.
Namba tatu: Mvutano
Samuel Mwamkinga kutoka Tanzania amekuwa mshindi wa tatu. Mchoro wake umeweka wazi changamoto za Umoja wa Afrika.
Mbwa anaebwaka hawezi kuuma
Baadhi ya washiriki wa mashindano hayo wanaonesha nafasi ya Afrika katika siasa za kimataifa. Miongoni mwa hao ni Ssentongo Jimmy Spire kutoka Uganda aliechora katuni iliyoitwa "Muungano kwa ajili ya usemi"
Mzigo mzito
Mchoro wa Junior Heritier Bilaka kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo vilevile unaelezea ushawishi mataifa yenye nguvu duniani kwa wanasiasa wa Afrika.
Kwa mwendo wa Konokono
Mtazamo wa Tayo Fatunia kwa maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja wa Afrika sio mzuri.
Afrika motoni
Picha hii imechorwa na Dick Esale kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Hatma ya kupendeza
Guelajo Sile kutoka Guinea Bissau miongoni mwa washiriki wachache katika shindano hilo ambae ameonesha mtazamo chanya kwa Afrika. Anaamini kwamba mwaka wa 2013 ni "Mwaka wa Afrika" na kauli hiyo ndio imebeba jina la mchoro wake.
Upya wenye mizizi ya zamani
Hivi ndivyo ambavyo Haswel Kunyunye kutoka malawi alivyoweza kuuelezea iliyokuwa Umoja wa nchi huru za Afrika (OAU) mpaka sasa Umoja wa Afrika (AU)
Africa ni kirago chenye viraka
Mchora katuni kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Michael Maloji M. Anaonesha mtazamo wake kuhusu Afrika
Msingi wa Umoja
"Miguu ya Afrika" ni jina la kielelelezo kilichowasilishwa na Siphiwo Sobopha kutoka Afrika Kusini. Michoro zaidi ya katuni inapatikana katika www.cartoon-competition.org.