Katumbi ataka kuungana na Bemba uchaguzi DRC
26 Juni 2018Matangazo
Bemba, ambaye anatarajiwa kurejea nchini mwake hivi karibuni, baada ya hukumu dhidi yake katika uhalifu wa kivita kufutwa kutokana na kukata rufaa.
Katumbi, Bemba na Felix Tshisekedi, kiongozi wa chama kikubwa cha upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ni wagombea wakuu,wa upinzani ambao wanaweza kugombea katika uchaguzi wa rais mwezi Desemba mwaka huu kumchagua mrithi wa rais wa sasa, Joseph Kabila.
Bemba, kiongozi wa zamani wa waasi mbaye ni maaruf na makamu wa rais aliondoka nchini Congo mwaka 2007, na ametumikia kifungo cha miaka 10 jela mjini The Hague. Lakini anatarajiwa kurejea nyumbani mwezi Julai na anaweza kushiriki katika uchaguzi.