1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Katibu Mkuu UN ataka mapambano zaidi ya hali ya hewa

12 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cag7

BALI.Katibu Mkuu wa Mataifa Ban Ki moon ametoa wito kwa nchi zote kukubaliana na mkataba wa kupambana na ongezeko la ujoto duniani ifikapo mwaka 2009.

Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alitoa wito huo huko Bali Indonesia katika mkutano wa umoja huo juu mabadiliko ya hali ya hewa.

Mawaziri wa Mazingira na wakuu kadhaa wa serikali watatumia siku tatu za mwisho za mkutano huo kujaribu kuweka muundo wa kupambana na mabadiliko ya hali hewa kabla ya mwaka 2012 wakati mkataba wa Kyoto utakapomalizika.

Waziri wa mazingira wa Ujerumani Sigmar Gabriel anategemwa kuhutubia mkutano huo mchana huu.

Mapema Waziri Mkuu mpya wa Australia Kevin Rudd alimkabidhi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, barua rasmi ya nchi hiyo kuridhia mkataba wa Kyoto na kuicha Marekani kuwa nchi pekee kati ya zilizoendelea ambayo haijauridhia mkataba huo, unaotaka kupunguzwa kwa gesi ya Carbon.