Kashfa ya pesa yachunguzwa na polisi wa London
30 Novemba 2007Matangazo
Polisi katika mji mkuu wa Uingereza,London wameanza rasmi kuchunguza kashfa ya pesa inayokihusisha chama cha Labour cha Waziri Mkuu Gordon Brown.Chama hicho kinyume na sheria, kilipokea mchango wa Pauni 600,000 za Kingereza kutoka kwa tajiri anaemiliki majengo,David Abrahams.
Uchunguzi huo unafanywa wakati ambapo umaarufu wa Brown umepunguka miongoni mwa wananchi.Hivi karibuni,uchunguzi wa maoni ya raia umeonyesha kuwa chama cha Labour kimepitwa na chama cha upinzani cha kihafidhina kwa pointi 11,hali ambayo haikupata kutokea tangu enzi ya waziri mkuu wa zamani wa kihafidhina Margaret Thatcher.