1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Karsai akaribisha upanuzi wa harakati za NATO.

7 Februari 2004
https://p.dw.com/p/CFgx
KABUL: Nchini Afghanistan Rais Hamid Karzai amekaribisha uamuzi wa Shirika la NATO wa kutanua harakati zake za kuhifadhi amani nchini humo. Kutanuliwa kwa harakati za Kikosi cha Kimataifa cha Kuhifadhi Afghanistan - ISAF - ni muhimu sana kwa ukarabati wna usalama wa Afghanistan, alisema Rais Karsai mjini Kabul. Hapo jana Mawaziri wa Mambo ya Ulinzi wa NATO waliwafikiana katika mkutano wao mjini Munich kupeleka wanajeshi wake pia sehemu za mikoani na kukuimarisha kikosi kilichopo Afghanistan. Hadi sasa ni wanajeshi 200 tu wa Kijerumani waliowekwa mjini Kundus chini ya amri ya kikosi cha ISAF na NATO. Wanadiplomasia wamearifu kuwa hivi sasa nazo Uingereza, Uitalia, Uholanzi, Norway na Uturuki zinataka kupeleka wanajeshi wao Afghanistan.