1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Karibu watu 40 wafa katika mlipuko wa bomu, Pakistan

30 Julai 2023

Karibu watu 40 wamekufa na wengine wengi kujeruhiwa hii leo baada ya bomu kulipuka katika mkutano wa kisiasa wa chama cha siasa kali za Kiislamu kaskazinimashariki mwa Pakistan.

https://p.dw.com/p/4UZ0s
Pakistan Bajur | Bombenschlag auf politishce Veranstaltung
Gari ya kubebea wagonjwa ikiwa imebeba waliojeruhiwa kwenye tukio hilo la bomu nchini Pakistani, Julai 30, 2023.Picha: Rescue 1122 Head Quarters/AP/picture alliance

Inspekta Jenerali wa polis Akhtar Hayat Gandapur amesema bomu hilo lililipuka kabla kiongozi wa ngazi za juu wa chama hicho aliyetakiwa kuhutubia mbele ya umati huo kuwasili.

Amesema mlipuko huo ulikilenga chama hicho cha Jamiat Ulema-e-Islam, kilichokuwa kinafanya mkutano mkuu katika mji wa Khar, karibu na mpaka wa Afghanistan, kuelekea uchaguzi baadae mwaka huu.

Afisa mwandamizi wa wilaya Anwar ul Haq, amethibitisha juu ya vifo hivyo, alipozungumza na shirika la habari la AFP.